Musk agoma kumchangia Trump, Biden

MKURUGENZI Mtendaji wa TESLA, Elon Musk amesema katika harakati za kuwania urais Joe Biden na Donald Trump hatochangia kiasi chochote cha pesa kwa mgombea yoyote.

“Ili tu kuwa wazi kabisa, sitoi pesa kwa mgombea yeyote wa Rais wa Marekani,” Musk alisema katika chapisho kwenye mtandao wa X.

‘Tweet’ ya Musk ilikuja siku moja baada ya gazeti la The New York Times kuripoti kwamba wikendi iliyopita alikutana na Trump na kile gazeti hilo lilichokiita wafadhili wachache wa Republican, huko Palm Beach, Florida nyumbani kwa rais huyo wa zamani Marekani.

Musk anashika nafasi ya pili katika orodha ya watu matajiri zaidi duniani, akiwa na wastani wa Dola bilioni 195, kulingana na Forbes.

Musk, ambaye pia anaongoza SpaceX, anaweza kumuunga mkono Trump au Biden kwa njia zingine ila sio mchango wa moja kwa moja katika kampeni zao.

Habari Zifananazo

Back to top button