Mussa Maulid meya mpya Kigoma Ujiji

KIGOMA; WAJUMBE wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamemchagua Diwani wa Kata ya Mwanga Kusini Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mussa Maulid kuwa Meya wa manispaa hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Maulid amechaguliwa nafasi hiyo kwa kupata kura 24 za ndiyo kati ya kura 25 za madiwani waliohudhuria baraza hilo. Kura moja ilisema hapana.

Msimamizi wa uchaguzi huo kwa niaba ya Katibu Tawala Wilaya ya Kigoma, Ofisa Tawala kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigoma, Dollar Buzaire pia alimtangaza Mgeni Kakolwa kuwa Naibu Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kupata kura 24 za ndiyo na kura moja ya hapana.



