Mussa Mwenyekiti mpya UVCCM Nyamagana 

MUSSA Abdallah ameibuka kuwa Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Nyamagana.

Msimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi, alimtangaza Mussa Abdallah kuwa mshindi, baada ya kupata kura 221 na mpinzani wake Boniphace Zephania, kupata kura 155 katika kura 387 zilizopigwa.

Makilagi alitangaza matokeo hayo jana usiku, wakati wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Butimba, mkoani Mwanza.

Makilagi aliwashukuru wajumbe kwa kufanya uchaguzi wa uhuru na haki na kumtaka Mwenyekiti mpya Mussa Abdallah na Mwenyekiti alipita Boniphace Zephania kumaliza tofauti zao na kujenga chama imara.

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana, Ramadhan Omary, amesema  uchaguzi ulikuwa hhuru na haki.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo mpya, aliwataka vijana wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba uchaguzi umeisha na wote sasa ni kitu kimoja.

“Makundi sasa yaishe, tunachotakiwa vijana wenzangu kwa sasa tufanye kazi kwa bidii na kujenga chama chetu,” amesema Abdallah.

Aliwashukuru wapiga kura kwa kumchagua kuwa Mwenyekiti na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na viongozi wapya pamoja na wale waliomaliza muda wao.

Habari Zifananazo

Back to top button