Muswada Bima ya Afya kujadiliwa bungeni kesho

SERIKALI inatarajia kurejea bungeni tena hapo kesho Novemba 1,2023 na Muswada wa Bima ya Afya kwa wote.

Awali muswada huo ulikwama mwezi Februari 2023 kwa hoja iliyotolewa na Bunge ya kutokuwepo kwa chanzo endelevu cha fedha kutekeleza mpango huo.

Muswada huu ni ndoto ya serikali ya miaka mingi ambapo Serikali ya  Rais Dk Samia Suluhu Hassan imeboresha huduma bora za afya kuanzia ngazi ya taifa hadi ya msingi kwa kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora za afya karibu zaidi na maeneo yao.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya, Englibert Kayombo amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya, wadau wa sekta na wataalam wengine tayari wamefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Bunge pamoja na wadau, hata hivyo semina zimefanyika kwa makundi mbalimbali ndani ya jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya kwa wote .

“Tulipokea maoni yao na kuyafanyia kazi wananchi kesho watege macho na masikio yao Bungeni kujua nini ambacho Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu atawasilisha bungeni” amesema.

Amesema kuwa kupitishwa kwa muswada huu kutawezesha kila Mtanzania kuwa ndani ya mfumo wa Bima ya Afya hatua itakayoboresha zaidi upatikanaji wa huduma za matibabu bila kuwa na kiwazo cha fedha.

“Serikali yetu ni sikivu sana na imefanyia kazi hoja zote zilizoibuliwa na Waheshimiwa Wabunge ambao ndio wawakilishi wa wananchi hivyo yaliyomo ndani ya muswada huo yamelenga kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya bila ya kikwazo cha fedha.” amesema  Kayombo.

Kuhusu gharama za vifurushi, Kayombo amesema kuwa mara baada ya Muswada huo kupita na kuwa sheria, kanuni zitatungwa ili kuratibu suala ya gharama za vifurushi na kusema kuwa uchambuzi utafanyika ili vifurushi viwe vya gharama nafuu na kila Mwananchi aweze kuwa na bima ya afya.

Ameongeza kuwa kwa upande wa Serikali imeshakamilisha maandalizi ya kutoa huduma kwa wananchi kupitia mfumo wa bima ya afya kwa wote ambapo imeboresha ubora wa huduma katika vituo vyake vya kutolea huduma ikiwemo upatikanaji wa dawa,  ununuzi na usimikaji wa vifaa na vifaa tiba, ajira za watumishi.

“Kwa sasa nchi yetu iko mbali sana katika utoaji wa huduma, tuna vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa magonjwa, huduma nyingi za kibingwa zinapatikana hapa hapa nchini lakini pia huduma za afya zimesogezwa sana kwa wananchi hivyo kama nchi tupo tayari kutekeleza hili, nia na uwezo wa kufanya hivyo tunao” amesema  Kayombo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
6 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU
1 month ago

Viboko 12 wakati unaingia JELA na viboko 12 wakati unatoka ukamsimulie mkeo!

Jamii yaungua kwa ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU YA PANYA 500 na kukimbizwa hospitali na kuruhusiwa na Daktari

Capture.JPG
Kathyalter
Kathyalter

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 1 month ago by Kathyalter
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUM
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUM
Reply to  Kathyalter
1 month ago

THE KINGDOM IDEOLOGY WILL BE ESTABLISHED THROUGH A NEW CONSTITUTION… WHAT KIND OF TRIBE DO YOU THINK HE’S GOING TO COME FROM?

Capture.JPG
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU
1 month ago

Viboko 12 wakati unaingia JELA na viboko 12 wakati unatoka ukamsimulie mkeo!

Jamii yaungua kwa ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU YA PANYA 500 na kukimbizwa hospitali na kuruhusiwa na Daktari…

Capture.JPG
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU
ULIKUWA NA MRADI/PROJECT YA MATRILIONI WAKATI SUMU
1 month ago

SERIKALI YA WANYONGE MWAKA 2220
1. Toyota Alphard 2021 White in Kinondoni – Cars, George Mahimbo | Jiji.co.tz
2. Land Rover Range Rover Vogue 2021 Black in Kinondoni – Cars, thebluesanthonio | Jiji.co.tz
3. Land Rover Range Rover 2019 Burgundy in Kinondoni – Cars, Jm Motors Vigo | Jiji.co.tz
4. BMW X5 2008 White in Kinondoni – Cars, George Mahimbo | Jiji.co.tz
5. BMW X5 2007 Gray in Kinondoni – Cars, Cars Guru Tanzania | Jiji.co.tz
6. BMW X5 2015 White in Kinondoni – Cars, Franklin Carsforyou | Jiji.co.tz
7. BMW R-Series 2022 Blue in Kinondoni – Cars, Andrew Kingo Jr | Jiji.co.tz
8. Land Rover Range Rover Sport 2014 Blue in Kinondoni – Cars, Ndingabeipoa Tz | Jiji.co.tz
CAR Repair Home Services 24 Hours
ELIMU BURE/BILA MALIPO

Capture.JPG
Angila
Angila
1 month ago

Start your home business right now. Spend more time with your family and earn. Start bringing 99Dollars per hr just on a computer.(Qr) Very easy way to make your life happy and earning continuously…
.
.
.
This is where i started…>> http://remarkableincome09.blogspot.com

Back to top button
6
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x