Muswada bima ya afya kwa wote wakwama

MUSWADA wa Bima ya Afya kwa Wote (UHC), ambao ulikuwa uwasilishwe bungeni leo Alhamisi Februari 9, 2023 jijini Dodoma umekwama kwa mara nyingine.

Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge iliyotolewa Januari 30, 2023, ulionyesha muswada huo ulikuwa uwasilishwe bungeni leo kwa hatua zake zote tatu za mchakato wa utungwaji wa sheria.

Akizungumza Spika wa Bunge Tulia Ackson amesema Muswada huo ulikua uwasilishwe bungeni leo lakini kuna vipengele ambavyo bado havijakamilika hivyo hautawasilishwa.

“Muswada huu ulikuwa ujadiliwe bungeni leo na kesho, umerudishwa kwenye kamati kwa ajili ya kujadiliwa zaidi na kisha utaletwaq Bungeni katika mikutano inayofuta, majadiliano yanaendelea hasaq eneo la bajeti na utekelezaji.

Hii ni mara ya pili muswada huo kukwama tangu usomwe kwa mara ya kwanza bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge na kupelekwa katika kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kuchambuliwa.

Awali muswada huo ulipangwa kujadiliwa Novemba 12, 2022 katika mkutano wa tisa wa Bunge, lakini ulikwama.

Muswada huo sasa utawasilishwa katika Bunge la Aprili. Bunge linahairishwa kesho.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x