Muswada Sheria ya Ununuzi wa Umma watua bungeni

Waziri wa Fedha ,Dk Mwigulu Nchemba.

SERIKALI leo Septemba 7, 2023 imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa mwaka 2023.

Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema wakati akiwasilisha muswada huo bungeni lengo la muswada huo ni kuweka masharti bora ya usimamizi wa ununuzi wa umma, ugavi na uondoshaji wa mali kwa njia ya zabuni.

“Kwa ujumla, sheria inayopendekezwa inakusudia kutatua changamoto zilizobainika katika utekelezaji wa masharti na taratibu za ununuzi, ugavi na uondoshaji wa mali kwa njia ya zabuni,” amesema Waziri Nchemba na kuongeza kuwa:

Advertisement

“Mheshimiwa Spika, Madhumuni ya muswada huu ni: Kwanza kufangamanisha masuala ya ununuzi na ugavi katika mnyororo wa usimamizi wa ugavi;

“Pili, kuimarisha mazingira ya ununuzi na ugavi kwa taasisi na mashirika ya umma yanayojiendesha kibiashara, Tatu; kupunguza muda katika hatua na michakato ya zabuni.”

3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *