Mutungi asifu wingi wa wanawake katika siasa

MSAJILI wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi amesema ushiriki wa wanawake katika siasa umekua ukipiga hatua kila mwaka licha ya uchache wa nafasi za wanawake katika ngazi ya kutoa maamuzi.

Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jumanne Aprili 25 Jijini Dar es salaam  wakati wa uzinduzi wa warsha ya kupitia ripoti ya uchambuzi wa mapengo ya kijinsia katika nyaraka za kisera za vyama vya siasa ambapo alibanisha kuwa wanawake wana nafasi  ya kushiriki katika nafasi za kutoa maamuzi na kukuza demokrasia hapa nchini.

Advertisement

Jaji Mutungi amesema kuwa wanawake wana mchango mkubwa katika vyama vya siasa na maendeleo ya demokrasia kutokana na wingi wao hivyo kuna haja ya kuwa  na uwiano sawa wa nafasi za uongozi unaozingatia jinsia.

Aidha Jaji Mutungi amewataka wanawake kuwa na umoja na kuacha misuguano ya kisiasa wao kwa wao kwani hurudisha nyuma maendeleo ya ushiriki wa wanawake katika siasa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF na Makamu Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD)  Profesa Ibrahim Lipumba amesema mkutano huo umelenga kuangazia ushiriki wa wananawake katika kujenga mfumo wa demokrasia hapa nchini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *