“Mvomero Tutunzane 2023” yaanza kutekelezwa

SERIKALI ya Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro imeanza utekelezaji wa kampeni ya kihistoria ya “Mvomero Tutunzane 2023”.

Kampeni hiyo ina lengo la kuhamashisha kilimo cha zao la ufuta na kulifanya la kimkakati kutokana na soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Kampeni hiyo pia imelenga kuhamashisha wafugaji kujitokeza kulima na kupanda malisho ya mifugo kufunga kisasa ili kuwa na mifugo yenye ubora mkubwa unaohitajika kwenye soko ya kitaifa na kimataifa ikiwa na kuondokana na migogoro baina yao na wakulima.

Mkuu wa wilaya hiyo ,Judith Nguli alisema hayo katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya hiyo wakati akitambulisha kampeni hiyo kwneye kikao cha wakulima na wafugaji na wataalamu wa ugani.

Nguli alisema kuwa kampeni hiyo pia imelenga kuleta ushirikiano umoja, upendo na mshikamano baina ya wakulima na wafungaji hali ambayo itasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa migogoro.

Mkuu wa wilaya alisema katika utekelezaji wa Kampeni hiyo malumu itahusisha Kata tano za wilaya ambazo ni Dakawa, Mkindo, Mangae , Lubungo na Melela.

Alisema kwenye kupanda wa malisho itahusisha kata ya Dakawa katika kijiji cha Wami Luhindo , Wami Sokoine na Dakawa , kata ya Mkindo ni kijiji cha Kamabara , Kata ya Mangae ni kijiji cha Mela , kata ya Lubungo ni kijiji cha Vihansi ambavyo baadhi ni vya wafufaji na vingine vinajukuisha wakulima na wafugaji.

Alisema kampeni hiyo itatoa elimu na kuwahamasisha wafugaji kulima na kupanga manyasi ya malisho ya mifugo yao, kuchimba marambo na visima kwa ajili ya mifugo yao hali ambayo itasaidia kuiweka Mvomero katika hali salama.

Kwa upande wa kilimo cha ufuta alitaja kata zitakazo husishwa na kampeni hiyo ni Doma , Mangae , Msongozi , Lubungo na Melela ambazo vijiji vyake vipo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Mikumi na vinakabiliwa zaidi ya changamoto za wanyamapori wakali na wakaribifu hasa Tembo.

“Tuliashaanza maandalizi ya awali tangu Julai mwaka huu (2023) na sasa kunaelekea kuzindua jukwaa la Kampeni ya Kihistoria ya Mvomero Tutunzane 2023 Oktoba 4, 2023 “ alisema Nguli

Hivyo alisema ,baada ya kuzinduliwa kwa jukwaa hilo na kabla ya kuanza mwezi Novemba au Desemba kampeni hiyo itaanza rasmi ya kwenda kupanda malisho mashambani pamoja na zao la ufuta kwa mashamba ya wakulima kilimo .

“ Orodha ya mashamba binafsi imepatikana ambayo imewasilishwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi , wizara ya Mifugo na Uvuvi , Ofisi ya Rais Mazingira na Wizara ya Fedha na nyingine mtambuka ili kuofanya kampeni hii kuwa imefuata misingi yote ya kisheria’ alisema Nguli

Katika kufanikisha kampeni hiyo aliwahimiza wakulima, wafugaji na wananchi wote kutunza mazingira na vyanzo vya maji na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya mita 60 kutoka kwenye chanzo cha maji.

Habari Zifananazo

Back to top button