DAR ES SALAAM: UBUNIFU na usasa humsaidia mwanadamu kuvumbua njia kadha wa kadha ili kutatua adha na changamoto zinazomkabili katika mazingira yake.

Pichani ni mtoa huduma ya usafiri wa bodaboda mtandaoni akitumia mwavuli maalumu wa kukinga kifaa chake cha kazi (simu ya mkononi) dhidi ya mvua zinazoendelea jijini Dar es Salaam.

Ubunifu na usasa unamfanya kuendelea kuhakikisha huduma ya usafiri kwa wateja wa katikati ya Jiji, Posta Dar es Salaam zinaendelea ilhali kitendea kazi nacho kingali salama salimina.