WATUMIAJI wa barabara ya kwenda Mto wa Mbu hadi Makuyuni wamesimama kwa saa kadhaa kusubiri maji kupungua ili kupita huku vijana wakijipatia ajira ya chapuchapu
Ajira hiyo za chapuchapu imetokea eneo la Esilalei wilayani Monduli mkoani Arusha asubuhi ya leo Desemba 23, 2022 kwa vijana hao kusukuma magari madogo kwa shilingi 5,000 na makubwa kwa shilingi 10,000
Madereva wamelazimika kuzima magari na kutoa hela ili kuvushwa kwa kusukumwa.
“Bila hela hupiti hapa na bodaboda yenyewe unatoa shiinig 1,000 na mtu tunamvusha kwa shilingi 500.
“Amesema Jumanne Juma, mmoja wa vijana wavushaji na kuongeza
“Mvua imetupa fursa kwetu tunashukuru tunavusha magari, watu tujipatie riziki zetu tunatamani maji yasipungue.”Amesema
Comments are closed.