Mvua yaleta balaa Bukoba

KAGERA; Bukoba; Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha alfajiri ya leo Oktoba 18, 2023, imesababisha madhara katika maeneo mbalimbali Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Kutokana na hali hiyo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Siima amewaagiza watendaji wa serikali za mitaa na kata Manispaa ya Bukoba kuhakikisha wanashirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa kufanya tathimini kujua athari za mvua hizo kwa jamii.

Pia ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani Kagera kufanya uchunguzi wa mtu aliyekutwa amekufa katika Manispaa ya Bukoba, ili kubaini kama kifo icho kimetokana na mvua hizo au la.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema baadhi ya nyumba zimeathriwa na mvua hiyo, pia vibanda vya biashara pamoja na mazao ya mboga mboga yameguswa na mvua hizo.

Hata hivyo amesema kwa muda mfupi hawawezi kutoa tathimini ya athari za mva, lakini kupitia watendaji wataweza kupata tathimini ya jumla na kufahamu athari ikiwemo za miundombinu.

Ametaka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu mvua hizo, lakini pia watoe taarifa sahihi pale timu ya tathimini itakapofika, akisisitiza kuwa lazima wananchi waendelee kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kupitia vyombo vya habari.

Viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa Jimbo la Bukoba Stephen Byabato, madiwani na viongozi wengine wameonekana mitaa mbalimbali wakitembelea wananchi waliopata madhara mbalimbali kwa kutoa pole, huku viongozi wengine wakituma ujumbe wao kupitia majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button