MTWARA: MVULANA mmoja (14) mkazi wa kijiji cha Mnete Kitongoji cha Chiano Kata ya Nalingu iliyopo halmashauri ya Wilaya ya Mtwara anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma kunajisi watoto wawili wanaodaiwa kuwa ni wa familia moja.
Akitoa taarifa hiyo jana kwa waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Nicodemus Katembo – ACP amesema Oktoba 1, hadi Oktoba 15, 2023 mtuhumiwa wa tukio hilo anayedaiwa kuwa ni kaka wa watoto hao alifanya tukio kwa nyakati tofauti.
amesema alimbaka mtoto wa kike (7) na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri na kisha kumnajisi mtoto wa kiume (5) na kumsababishia maumivu katika sehemu yake ya haja kubwa ambapo wote ni wakazi wa kata hiyo.
Amesema kiini cha tukio ni tamaa za kimwili hivyo ametoa rai kwa wananchi mkoani humo, kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kupinga unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pamoja na maadili yanayo kinzana na sheria za nchi.
Mama mzazi wa watoto hao anaelezea namna alivyopokea taarifa hizo‘’wakati nipo kazini mama alinipigia simu kuniambia njoo nyumbani huku watoto wamevamiwa, nikauliza na nani….wewe njoo tu utajua hapo hapo nikatoka kazini nakaja hapa nyumbani nikauliza mtu wenyewe aliyefanya hivyo ni nani akanambia ndugu yako unayekaa naye ndani’’,amesema
Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Halima Mohamed amesema alipopata taarifa hizo mtuhumiwa alikamatwa na kufikisha ofisini hapo, alipohojiwa alikiri kufanya tukio hilo.
Comments are closed.