RAIS Samia amesema kufikia 2030 anataka asilimia 88 ya wanawake Tanzania watumie nishati safi.
Kiongozi huyo wa nchi ameeleza hayo leo Machi 13, 2024 alipotoa maagizo kwa Christina Mndeme aliyeteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) katika gafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
“Kuna ‘project’ (mradi) ya clean cooking kwa wanawake wa Afrika, lazima tuoneshe mfano hapa nyumbani, kanisaidie tuanze hapa tuoneshe mfano,”
“Mimi nakwenda kutumika kwa Afrika, lakini hapa ni wewe na mshauri wangu ndani ya ofisi yangu na wengine mtakaofanya nao kazi kwenye mazingira,”amesema Rais Samia.