Mwakinyo afungiwa mwaka mmoja

KAMISHENI ya ngumi za kulipwa nchini (TPBRC) imemfungia bondia Hassan Mwakinyo mwaka mmoja.

Mwakinyo amefungiwa kupanda ulingoni ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya Sh milioni 1.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPBRC, Mwakinyo amefungiwa kutokana na kugomea pambano lake lililokuwa lifanyike Septemba 29 mwaka huu.

Habari Zifananazo

Back to top button