Mwakinyo agomea pambano la kesho

BONDIA Hassan Mwakinyo amesema hatopanda ulingoni kupigana dhidi ya Bondia Julius Indonga kwenye pambano la kuwania mkanda wa IBA International kesho.


Mwakinyo amesema uamuzi huo umetokana na uwongo na udanganyifu wa Mapromota.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mwakinyo ameandika kuwa “Kwetu kama wachezaji wa ndani naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uwongo na udanganyifu, wa ma promota binafsi sina tatizo na mtu ila pia naheshimu sana kazi yangu na siko tayari kuona watu wana nijaribu au kutaka kuharibu jina langu,” Ameandika Mwakinyo.

“Napenda sana Kushukuru M/mungu kwa uzima na afya nilio nayo leo” pia niwashukuru sana washabiki zangu kwa kujitokeza kwa nguvu kuonyesha shauku ya kuniunga mkono nawashukuru sana.” ameongeza.

Advertisement
3 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *