Mwakinyo kuzichapa Dodoma Apr.23

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano la kampeni ya kuchangia  taulo za watoto wa kike litakalofanyika Aprili 23 mwaka huu, mkoani Dodoma kati ya  Hassan Mwakinyo na Kuseva Katembo kutoka Afrika Kusini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, promota wa pambano hilo, Sophia Mwakagenda amesema litakuwa na raundi 10 lisilo la ubingwa na kwamba fedha zitakazopatikana zitasaidia kununua taulo za kike.

“Fedha hizi tutanunua taulo za kike kwa kusaidia mabinti wetu Mikoa ya Njombe, Mbeya, Ruvuma na Iringa, “amesema.

Bondia, Hassan Mwakinyo amesema amejiandaa vizuri na bado anaendelea kujifua kwa lengo la kuonesha mchezo nzuri siku hiyo.

Mwakinyo ametoa wito kwa serikali kuunga mkono pambano hilo pamoja na mchezo huo, ili mabondia kufanya vizuri zaidi.

“Nimejipanga kufanya vizuri kushinda pambano hili, wadau na mashabiki wangu wategemee kuona mchezo nzuri kutoka kwangu, “amesema Mwakinyo.

Mwakinyo alieleza kuwa ni jambo kubwa kuwepo kwa mgeni rasmi Waziri wa Mkuu, jambo ambalo litampa nguvu ya kupambana dhidi ya mpinzani wake.

Pamoja na pambano la Mwakinyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi matano, ambayo ni Jesca Mfinanga dhidi ya Salma Ally, Feriche Mashauri atapimana na Rukia Nasirite , huku Halima Bandola atapigana Sarafina Julius, Happy Daudi atapigana na Hawa Stanford na Yonas Segu atapimana nguvu na Ibrahim Majibu

Habari Zifananazo

Back to top button