Mwakinyo mwanamichezo bora wa mwezi

Bondia Hassan Mwakinyo ametunukiwa tuzo ya mwanamichezo bora wa mwezi Januari.

Utoaji wa tuzo hizo umefanyika jana katika tamasha la Michezo lililoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA) katika viwanja vya Msasani Beach Club, jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwakinyo amesema ni fahari kwake kupokea tuzo hiyo ambayo inaonesha namna juhudi zake zinathaminiwa.

Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alimwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

TASWA imerejesha tuzo hizo ambazo kwa kitambo hazikuwa zikifanyika ila zimerejeshwa tena chini ya Mwenyekiti wa sasa wa TASWA, Amiry Mhando.

Habari Zifananazo

Back to top button