Mwamba Ancelotti hashikiki

Kila mechi rekodi

MADRID: Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameandika historia mpya katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwa kocha wa kwaza kufikisha michezo 200 ya michuano hiyo.

Kocha huyo amefikisha rekodi hiyo akiwa amefundisha timu nane zilizoshiriki Ligi ya Mabingwa katika nyakati tofauti timu hizo ni Parma, Juventus, AC Milan, Chelsea, Bayern Munich, PSG, Napoli na Real Madrid.

Katika michezo hiyo 200 kocha huyo ameibuka na ushindi mara 114.

Katika adhimisho lake la mchezo wa 200 jana usiku timu yake ya Real Madrid ililazimishwa sare ya 3-3 na Manchester City.

Ni Makocha tisa pekee waliosimamia michezo zaidi ya 100 kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya,

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson anafuatia akiwa na michezo 190, huku kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger akiwa na michezo 178.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesimamia michezo 168 huku Jose Mourinho akifuatia na michezo 145 miongoni mwa wengine 

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesimamia michezo 168 huku Jose Mourinho akifuatia na michezo 145 miongoni mwa wengine kwenye michuano hiyo yenye hadhi zaidi kwa ngazi ya vilabu barani Ulaya.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button