Mwamba huyu hapa Arusha

ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha (RC), Paul Makonda amewasili mkoani Arusha. Amepokelewa na viongozi wa serikali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa huo, Missaile Mussa pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo, Felician Mtahengerwa.

RC Makonda amewasili asubuhi hii na kisha msafara kuanza kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwaaajili ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella ambaye kwasasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)

Akiwa njiani magari na watu mbalimbimbali walisimama kupisha msafara huo huku wengine wakisema karibu mkuu wetu, Arusha tunakutegemea.

Advertisement