ZURICH: Mwamuzi Beida Dahane kutoka Maurtania ni miongoni mwa waamuzi 12 kutoka Afrika waliojumuishwa kwenye jopo la waamuzi watakaosimamia sheria za kandanda katika michezo ya Olimpiki ya baadae mwaka huu.
Mwamuzi huyo atakumbukwa mno na wapenda soka hasa mashabiki wa Yanga kutokana na tukio la utata katika mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns uliopigwa nchini Afrika Kusini juma lililopita.
Mpira uliopigwa na Stephan Aziz Ki ulidhaniwa kuwa goli lakini mwamuzi huyo alitoka na maamuzi ya tofauti na kuamuru hakuna goli ,maamuzi yaliyopigwa na wanazi wa soka kutoka sehemu mbalimbali ulimwenguni.
Kujumuishwa kwa mwamuzi huyo katika michuano hiyo inayotarajiwa kutimua vumbi baadae mwaka huu jijiji Paris nchini Ufaransa kumetafsiriwa kuwa ni imani waliyonayo Shirikisho la Mpira wa Miguu ulimwenguni ( FIFA) juu yake.