Mwanafunzi kidato cha kwanza Kahama hajulikani alipo

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Bulyanhulu Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga Neema Mpiga (14) amedaiwa kutoroka nyumbani saa sita usiku walezi wake hawafahamu alipo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kaka wa mwanafunzi huyo Paul Mpiga alisema alitoroka nyumbani tangu Septemba 2023 mpaka leo hajaonekana ambapo tayari ametoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji na jeshi la polisi kuwapa RB namba 1777/2023.

Mpiga alisema maelezo aliyopewa na mke wake kuwa mdogo wake ametoroka nyumbani usiku majira saa sita waligundua wakati mtoto wa miaka mitatu akilia huku akiwa peke yake wakati huwa wana lala wote kwenye chumba kimoja.

“Tumefanya jitihada za kumtafuta kila eneo hajaonekana na alitoroka alikuwa hana ugomvi na mtu yoyote tumekuwa tukiishi naye vizuri.”alisema Mpiga.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Mkolani ambapo anaishi mwanafunzi huyo Abasi Petro alisema kweli taarifa ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo zimemfikia amekuwa akifanya jitihada za kushirikiana na walezi wake kumtafuta.

“Kesi za kutoroka kwa mabinti zimekuwa zikiripotiwa mara kwa mara ndani ya mwezi mmoja utakuwa kesi mbili au tatu wengine wanapatikana na wengine hawapatikani”alisema Petro.

Mkuu wa shule ya sekondari hiyo John Masasi alisema kweli ni mwanafunzi wa shule hiyo ametoweka hajulikani alipo na ana miezi miwili haonekani alipo.

Ofisa ustawi wa jamii Richard ng’ondya alisema zipo taarifa za wasichana wanao toroshwa na wengine kutoroka wenyewe hivyo jitihada zifanyike kwa kushirikiana na jamii ili kuweza kumpata msichana huyo isitoshe kuendelea kupinga vitendo vya ukatili.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button