Mwanafunzi Panda Hili apatikana

'Alikuwa kwa Baba Jose muuza mkaa'

SAA chache baada ya tangazo la Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera la kutoa kitita cha sh milioni tano kwa atakayefanikisha kupatikana kwa mwanafunzi Ester Mwanyilu wa kidato cha tano shule ya Sekondari Panda Hili, mwanafunzi huyo amepatika maeneo ya Mbalizi.

Sauti inayoelezwa kuwa ni ya mama mzazi wa mtoto huyo anasema  kuwa Esther amepatika maeneo ya Mbalizi ambako alikuwa akiishi kwa mama mmoja ambaye ni fundi cherehani.

“Alivyotoroka shule alikwenda kwa huyo mama na  alibadilisha mavazi akawa anavaa Hijabu zile za kininja za kufunika uso na kubakiza macho tu na jina alibadilisha akawa aitwi tena Esthet anaitwa Erica.”Amesema na kuongeza

“Baada ya taarifa kusambaa na picha yake, kuna mtoto wa mama yake mkubwa (Esther), alikuwa anaongea na binti mmoja kuhusu kupotea kwa Esther, huyo binti akasema mbona huyo binti unayemsema kuna mahali nimemuona yuko  kwa mama mmoja Mbalizi lakini aitwi Esther anaitwa Erica.

Sauti ya mama mzazi wa Esther 

“Alipoangalia picha akasema ni yeye kabisa..ni yeye..pamoja na kwamba anajifunika tunashindwa kumtambua lakini ni yeye.

“Sasa yule binti mtoto wa mama yake mkubwa akaenda kumueleza mama yake mzazi, mama ake akaenda Polisi kutoa taarifa leo asubuhi Polisi wameenda kuzingira hiyo nyumba na walimkuta kweli Esther wakamkamata na uyo mama akakamatwa kwa ufupi taarifa nilizopata ndio hizo kutoka kwa babu yake na Esther mzaa mama.”Amesema mama uyo.

Mwanafunzi huyo alipotea tangu Mei 18, 2023  na jana  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliagiza uchunguzi wa kina ufanyike ili mtoto uyo aweze kupatikana

KAMANDA WA POLISI AZUNGUMZA:

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amesema Mwanafunzi  huyo wamemkamata maeneo ya Ifisi, Mbalizi Mbeya na alipelekwa maeneo hayo na  mfanyabiashara wa mkaa aliyefahamika kwa jina la Baba Jose.

Kamanda Kuzaga amesema ” leo majira ya Saa tano na dakika 30 amepatikana Ifisi katika mji mdogo wa mbalizi baada ya timu ya makachero iliyoongozwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya na Ofisi yangu.”Amesema Kuzaga na kuongeza

“Mwanafunzi huyu ambaye alikuwa akichukua mchepuo wa masomo ya sayansi yaani PCB alikutwa kwa mwanamke anaitwa Hazrati Abduli (24) ambaye alisema binti huyo alipelekwa kwake na mteja wake ambaye uwa anamletea magunia ya mkaa gengeni amemtaja kwa jina moja la Baba Jose.

“Baba Jose alimwambia Hazrat kuwa binti huyo ni mke wake na anaomba ampe hifadhi kwa muda na kwamba anatafuta chumba cha kupanga ili waishi wote, na atakapopata atakuja kumchukua, alimpokea  bila kujua, akamuliza binti jina lake ni nani akasema Erica na ametoka Morogoro hivyo akaendelea kukaa kwa uyo mama.

APIMWA MIMBA

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema wamempima Esther kipimo cha mimba ili kujua hali yake na majibu yameonyesha hana mimba.

“Tunaendelea kumfuatilia na siku zijazo tutampima tena, ikionyesha ana mimba tutampa nafasi ya kwenda kujifungia na kurudi shule.’Amesema

 

 

 

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button