Mwanafunzi SAUT afia mapangoni

NYAMAGANA, Mwanza: MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agostino (SAUT) cha jijini Mwanza, Boaz Sanga amekutwa amefariki dunia baada ya kuzama katika Ziwa Victoria mnamo Mei Mosi mwaka huu.

Taarifa iliyochapishwa leo na akaunti ya mtandao wa Instagram ya chuo hicho imeeleza kuwa, Sanga alikuwa mwanafunzi wa kitivo cha Elimu SAUT.

“Boaz Sanga amefariki dunia baada ya kuzama majini wakati akiogelea maeneo ya Sweya, Wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza,” Imeeleza taarifa hiyo.

“Taarifa za awali zilizotelewa, zoezi la kumtafuta lilianza jana usiku bila mafanikio,” imeeleza taarifa hiyo.

Akielezea namna mchakato wa uokoaji ulivyofanikiwa, Kamanda Zimamoto na Uokoaji jijini Mwanza, Kamila Laban amesema maaskari wabobezi wa uzamiaji wa jijini humo walipata mwili wa Sanga katika ukiwa umekwama katika mapango ya ziwa hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button