Mwanahabari auawa Msumbiji

MWANDISHI wa habari kutoka Msumbiji, João Chamusse amekutwa ameuawa eneo la nyumba yake nje kidogo ya mji mkuu Maputo katika tukio linaloshukiwa kuwa ni mauaji.

Vyombo vya habari vya nchini humo vimeeleza tukio hilo limefanywa na watu wasiojulikana na kwamba majirani walimsikia akipiga kelele kuomba msaada hatan hivyo hakuna aliyefanya hivyo.

Chamusse, mmiliki mwenza na mhariri wa Ponto por Ponto, gazeti binafsi la kila wiki la mtandaoni, alichangia maoni ya kukosoa serikali kwenye kituo cha televisheni nchini humo.

Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari inasema imefadhaishwa na mauaji ya mwandishi huyo na inatoa wito kwa mamlaka nchini Msumbiji kuchunguza kwa kina tukio hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button