Mwanamama ashinda Uwaziri Mkuu Uingereza

Waziri mkuu wa Uingereza, LIZ Truss

LIZ Truss amechaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza baada ya kumshinda mpinzani wake, Rishi Sunak kwa kupata kura 81,326 dhidi ya kura 60,399 katika kuwania uongozi wa Chama cha Conservative.

Truss aliyezaliwa Julai 26, 1975, alipata asilimia 57 ya kura zote halali zilizopigwa kumrithi Boris Johnson aliyejiuzulu Julai kutokana na kukumbwa na kashfa kadhaa.

Kiongozi huyo wa Uingereza anatarajiwa kushika rasmi uongozi kuanzia leo, huku taifa hilo likikabiliwa na changamoto za kiuchumi na kijamii.

Advertisement

Hata hivyo, katika hotuba yake fupi baada ya ushindi alioupata jana, Truss aliahidi kuja na mipango madhubuti ikiwamo ya kupunguza kodi, kujenga uchumi na kushughulikia matatizo yanayohusu nishati kwa ujumla wake.

Johnson atakapojiuzulu rasmi wadhifa wake kwa Malkia Elizabeth II leo, Truss naye atakwenda kuonana na Malkia na baada ya hapo atatakiwa kuunda serikali yake.

Mwanamama Truss alizaliwa katika mji wa Oxford na nyumbani kwake ni London na Norfolk. Pia ni Mbunge wa Jimbo la Norfolk Kusini Magharibi.

Anakuwa mwanamke wa tatu kushika wadhifa huo akitanguliwa na Margaret Thatcher na Theresa May.

 

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *