Aweka rekodi ya Guinness Mlima Kilimanjaro

Mwanadada mpiga kinubi maarufu duniani, Siobhan Brady kutokea nchini Ireland, leo Julai 25, 2023, ameweka rekodi ya dunia ya Guiness juu ya Mlima Kilimanjaro, Tanzania.

Siobhan ambaye alianza safari yake ya kupanda Mlima huo mrefu kuliko yote Afrika wiki iliyopita aliambatana na timu yake ya takribani watu 92.

Mwaka 2018 aliweka rekodi katika Mlima Himalaya, India wenye futi 16,000, sasa leo ameitangaza Tanzania zaidi na Mlima wetu Kilimanjaro kwa kuweka rekodi iitwayo “Guiness World Record for the Highest Harpist Concert” kwenye kilele cha juu zaidi duniani chenye futi 19,000 Uhuru Peak.

Muda nfupi uliopita mwanadada huyo alifanikiwa kupiga kinubi kwa dakika 34 na ili kuvunja rekodi alitakiwa kupiga kwa walau dakika zisizopungua 18 akichanganya nyimbo mbalimbali kutoka Ireland na mataifa mengine ya Ulaya.

Tukio hilo limerekodiwa na chombo kikubwa cha habari duniani The National Geographic.

Habari Zifananazo

5 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button