Mwanamuziki Whittaker afariki dunia

“Nenda sehemu yoyote kila mtu ana sehemu yake aliyozaliwa kwangu mimi ni Kenya” ni shairi linalopatikana kwenye wimbo wa ‘My land is Kenya’ ulioimbwa na msanii mzaliwa wa Kenya, raia wa Uingereza, Roger Whittaker taarifa mbaya amefariki dunia.

‘MY Land is Kenya’ ni wimbo uliotamba mwaka 1982 Wakenya walifarijika sana na wimbo huo hii leo wanahuzunika kumpoteza nguli huyo wa muziki aliyezaliwa Machi 22, 1936 jijini Nairobi na kufariki Paris, Ufaransa Jana.

“Ni kwa huzuni kubwa tunatoa habari za kifo cha Roger akiwa na umri wa miaka 87. Maisha yake, usanii na urithi wake umekuwa wa maana sana kwa watu wengi duniani kote,” rafiki yake, Jesse Waggoner, alichapisha kwenye ukurasa wa Facebook wa Whittaker.

Taarifa ya familia na tovuti yake rasmi, rogerwhittaker.com, ilithibitisha kwamba mwimbaji huyo wa lugha nyingi alifariki Septemba 13, 2023 katika hospitali iliyo kusini mwa Ufaransa ambako aliishi baada ya kazi yake ya kifahari iliyochukua zaidi ya nusu karne.

“Roger alikuwa msanii mashuhuri, mume na baba mzuri. Aligusa mioyo ya watu wengi kwa muziki wake katika maisha yake yote na ataishi katika kumbukumbu zetu kila wakati,” taarifa ya familia ilisema.

Kifo chake kinakuja takriban mwezi mmoja baada ya ukurasa wake wa Facebook kutangaza kuwa alikuwa mgonjwa. Alikuwa akipokea matibabu na huduma hospitalini.

Habari Zifananazo

Back to top button