Mwanasheria: Inshu ya Feisal kuweni na subira

Mwanasheria Fatma Karume anayemwakilisha mchezaji ya Yanga, Feisal Salum amesema wameiachia kamati itafakari upya maamuzi kuhusu mvutano wa kimkataba uliopo baina ya pande hizo mbili.

Karume amesema hayo leo Machi 2, 2023 akiwa katika viwanja vya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambapo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho hilo ilikuwa ikifanya mapitio, na kusema “wawe na subira.”

Kwa upande wa Yanga kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji, Andre Mtine imesema haina shaka na kwamba inasubiri jibu la mwisho la kamati.

“Tuliitwa kwenye review na tumekuja, tumesikilizwa na kusikiliza na sasa tunasubiri jibu la kamati tu,” amesema Mtine.

Kumbuka Yanga ilipeleka shauri kwenye kamati ikimtaka Feisal kutoa maelezo ya kuondoka ndani ya kikosi hicho kwa kuandika barua ya kuaga na kuichapisha katika ukurasa wake wa Instagram, Disemba 24,2022 bila mazungumzo.

Shauri hilo kwa mara ya kwanza lilisikilizwa Ijumaa ya Januari 6 mwaka huu na baada ya hapo TFF ilitoa barua iliyoeleza Feisal bado ni mchezaji halali wa Yanga kimkataba na kutoa nafasi ya upande wa Feisal kuomba mapitio ya shauri hilo kama hawataridhika na maamuzi yaliyotolewa.

Habari Zifananazo

Back to top button