Mwandishi HabariLEO ashinda tuzo za Orange

MWANDISHI wa habari Kampuni ya Mazageti ya Serikali (TSN) anayeandikia gazeti la  HabariLEO na Dailynews Digital, Aveline Kitomary ameibuka mshindi katika tuzo za ‘The Orange Award’ kwa kuwa mwandishi bora wa kike wa magazeti kwa mwaka 2024.

Mwandishi huyo ameshinda tuzo hiyo katika kipngele cha Best Female Newspaper personality of year 2024.

Advertisement

Tuzo hizo zilizotolewa na taasisi isiyo ya Serikali ya Dadahood iliyopo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kutambua mchango wa wanawake katika kuleta mabadiliko kwa jamii.

Utoaji wa tuzo hizo ulihusisha makundi mbalimbali kutoka katika vyombo vya habari ambavyo ni Redio, television, vyombo vya habari vya mtandaoni na magazeti.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo Kitomary aliishukuru taasisi ya Dadahood kwa kutambua mchango wake ndani ya jamii ikiwemo kuandika habari zinazoleta mabadiliko.

“Ninashukuru kwa kupata tuzo hii imekuwa chachu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutumikia taifa langu nawashukuru wote ambao wako mstari wa mbele katika kuhakikisha ninapata ushirikiano hasa kwa viongozi wangu wa gazeti la HabariLEO na Dailynews Digital,”amesema.

/* */