IMEELEZWA kuwa zao la mwani lina faida nyingi kiafya ikiwemo kuondoa kitambi. Kwa sababu hiyo jamii imeshauriwa kutumia zao hilo kwa ajili ya lishe na faida zingine.
Wakizungumza mkoani hapa ,wakulima kutoka kikundi cha Jionee cha wanawake wakulima wa mwani wanasema zao hilo pia linaweza kutumika kutengeneza juisi.
“Mwani una faida nyingi sana kiafya na kibiashara lakin bahati mbaya sana jamii yetu haIjatambua hilo. Mwani unasaidia kuondoa kitambi, kuongeza nguvu za kiume, mtu akiwa na mishipa ya ngili inasaidia sana, inatubu vidonda vya tumbu na kutibu asthma.” amesema mwenyekiti wa wakulima wa mwani kikundi cha Jionee kata ya Naumbu Halmashauri ya Mtwara Subira Muhibu.
Mkulima huyo amesema mwani kwa sasa unatumika kama zao la biashara tu hatua ambayo amesema sio rafiki katika kuongeza soko la mwani.
“Rai yetu jamii itambue umuhimu wa za la mwani hasa kwenye suala la afya watumie , wakifanya hivyo soko la mwani litapanda na litakuwa zao la muhimu na nguvu nyingi itaonekana,” amesema.
Mwani unatumila pia katika kutengeneza sabuni za kufulia na kuogea, bidhaa za utunzaji wa nywele na pia hutumika katika mlo kama virutubisho vya lishe.
Katika hatua nyingi, wakulima hao wameshukuru shirika lisilo la kiserikali la MSOAPO mkoani Mtwara kwa kuwajengea Kiwanda cha Kuchakata zao la mwani.
“Tunashukuru kwa kujengewa Kiwanda ambapo sasa tunatengeneza sababuni za kuongea za kufulia,” amesema.
Comments are closed.