Mwanyika, Mhagama wapitishwa uenyekiti Bunge

DODOMA; Bunge la Tanzania leo limeridhia na kuwapitisha wenyeviti wapya wa bunge waliopendekezwa na Kamati ya Uongozi ya Bunge.

Wiki iliyopita Kamati ya Uongozi ya Bunge ilipendekeza majina mawili kuchukua nafasi hiyo ya uenyekiti wa bunge, majina ambayo yalipendekezwa ni Deodatus Mwanyika ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda Biashara Kilimo na Mifugo na Dk Joseph Mhagama ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Utawala Katiba na Sheria.

Uteuzi huu mpya wa wenyeviti unakuja baada ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuwateua wenyeviti wa bunge, David Kihonzile kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Daniel Sirro kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi.

Advertisement

/* */