Mwanza kuwa kitovu cha utalii

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema jiji la Mwanza linatarajiwa kuwa kitovu cha utalii na kuwa na ongezeko la uwekezaji.

Pia kuwa na ongezeko la mnyororo wa. thamani wa mazao yatokanayo na utalii.

Masanja ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 46 Kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi(CCM) yaliyofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Advertisement

“Ninatambua kwamba pamoja na miradi inayotekelezwa katika Mkoa wa Mwanza, Sekta ya Maliasili na Utalii haijasahaulika na Mkoa wa Mwanza umependekezwa kuwa kitovu cha utalii” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amesema kuwa kutokana na miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan itaifanya Mwanza kufaidika na uwekezaji unaotokana na Sekta ya Utalii.

Amesema miradi ya ujenzi wa reli, stendi ya Nyegezi na Nyamhongolo, kiwanja cha ndege, Daraja la Magufuli la Kigongo-Busisi na miradi mingine itasaidia watalii kufika jijini Mwanza na hatimaye wananchi kufaidika na utalii.

“Tunatambua kuwa Rais Samia alizindua Royal Tour, hivyo kutokana na uwekezaji huo kila mwananchi anaguswa na mnyororo wa thamani unaotokana na utalii mfano mgeni anapokanyaga Mwanza wafanyabiashara wadogo watafaidika kama wauza machungwa, chakula na huduma za malazi.”

Amesema pia Serikali inamipango mikubwa na Mwanza na litakuwa ni jiji namba moja linalotambua uwekezaji unaotokana na Sekta ya Utalii.

Aidha , Masanja amewahimiza wananchi kuwa na tabia ya kupanda miti ili kuifadhi mazingira na kutunza uwepo wa hali ya hewa nzuri kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *