Mwassa atoa vyerehani 20 uwt

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwassa ametoa msaada wa vyerehani 20 vyenye thamani zaidi ya Sh milioni 10 kwa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) ili kuwawezesha kiuchumi.

Msaada huo umetolewa Februari 15,2023 ambapo amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao ya kiuchumi na wanaondokana na utegemezi.

Amesema vyerehani hivyo vitagawanywa kwa kila wilaya nane za kichama Kwa maana ya mbili kila wilaya wakati UWT mkoa ikipewa vinne na mpango huo ni kuwafikia wanawake wote hadi kwenye matawi.

Mbali na hayo ameahidi pia kutoa viwanja vitatu wanawake wa mkoa huo ili vijengwe viwanda vidogo ambayo wanawake wote bila kujali itikadi za vyama na wasio na vyama watapata fursa ya kufanya shughuli bila bughudha yoyote.

Mkuu wa mkoa pia amesema kuwa mkoa upo kwenye mpango mahususi wa kujenga soko la wanawake pekee kwa ajili ya kuwapa fursa ya kuuza mboga, matunda mazao ya viungo.

Kwa upande wake katibu wa UWT mkoa wa Morogoro, Grace Haule kwa niaba ya wanawake wa umoja huo amemshukuru mkuu na kuahidi kutumia vyerehani hivyo ukiwa mradi wao wa kiuchumi.

Habari Zifananazo

Back to top button