Mwema kuongoza bodi ya shirika la magereza

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewateua Mwenyekiti, Katibu na wajumbe 10 wa bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA).

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika wizara hiyo ilieleza kuwa Masauni amemteua Inspekta Jenerali wa Polisi (Mstaafu), Said Ally Mwema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza.

Taarifa hiyo kwa umma ilieleza ukwa pia Masauni amemteua Moremi Marwa kuwa Katibu wa bodi hiyo.

Wajumbe wa bodi walioteuliwa ni Emmanuel Akunay, Fuad Jaffer, Isaack Mazwile na Salim Aziz Salim. Wengine ni Theofilo Bwakea, Wanja Mtawazo, John Itambu, Raymond Mndolwa, Revocatus Rachel na Fatma Mangunda.

Katika hatua nyingine, Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ameteua viongozi wawili akiwamo Ali Said Bakari ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe katika Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale.

Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Zena Said ilimtaja mwingine aliyeteuliwa ni Zaituni Mohammed Haji ambaye amekuwa Katibu wa Tume ya Utumishi Serikalini katika Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora.

 

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button