MWIGIZAJI maarufu wa Kenya katika kipindi cha Vioja Mahakamani, Gibson Mbugua amefariki dunia.
–
Familia ya mwigizaji huyo aliyekuwa akijulikana kwa jina maarufu kama Mwendesha Mashitaka, imethibitisha kifo hicho na kusema kilitokea asubuhi leo kutokana na maradhi ya sukari na figo yaliyokuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.