Mwenge kukagua miradi 87 Tanga

TANGA; Mwenge wa Uhuru unaanza mbio zake leo mkoani Tanga, ukitokea mkoani Kilimanjaro na unatarajiwa kupitia mradi 87 yenye thamani ya Sh Bil 41 katika Halimashauri 11 za mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian amepokea mwenge huo leo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimamjaro Nurdin Babu katika uwanja wa Mazinde wilayani Korogwe, mkoani Tanga.