Mwenge kunogesha miradi 5 Mtwara

MIRADI ya maendeleo mitano yenye thamani ya shilingi bilioni 1.62 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, mkoani Mtwara itapitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2023.

Mratibu wa Mbio za Mwenge katika Halmashauri hiyo Nicholas Muya, amesema Mwenge huo utakimbizwa wilayani humo Aprili 3 na 4.

Ametaja miradi itakayopitiwa kuwa ni mradi wa maji, mradi wa barabara, mradi wa ufugaji wa kuku, shamba la mikorosho na mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike wenye mahitaji maalumu.

Advertisement

Nicholas amesema Halmashauri hiyo umejipanga vizuri kuhakikisha miradi yote itakayopitiwa inakidhi vigezo.

“Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara tumejipanga na bahati nzuri sehemu ya nyaraka tuko vizuri,” amesema.

Nicholas amesema halmashauri hiyo imeunda kamati ndogondogo kusimamia ununuzi, mipango na fedha kwenye miradi ambayo itapitiwa.

Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 kitaifa zitazinduliwa Aprili 2 mkoani Mtwara. Zaidi ya wageni 1000 kutoka nje ya Mkoa wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo ambazo zitafanyika katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Manispaa ya Mtwara Mikindani.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *