Mwenge wa Uhuru kukagua miradi ya Sh bilioni 1 Ukerewe

MWENGE wa Uhuru unatarajia kukagua miradi sita ya maendeleo katika Wilaya ya Ukerewe Mkoa wa Mwanza yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 1.

Mwenge wa Uhuru katika wilaya hiyo utafanya uzinduzi wa mradi wa ufugaji wa samaki Kasegenya, ujenzi wa mradi wa maji Kagunguli pamoja na ujenzi wa vyumba saba vya madarasa katika shule ya sekondari Ilangala.

Pia Mwenge wa Uhuru utakagua mradi wa Shamba la Matunda la Halmashauri pamoja na utengenezaji wa samani ya kikundi cha vijana cha ufundi ni ajira Nakatunguru.

Pia mwenge wa Uhuru utaweka Jiwe la Msingi katika kituo cha afya Murutilima.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button