Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi 17 Lushoto

MIRADI 17 yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 2 inatarajiwa kuzinduliwa, kukaguliwa na kuwekwa Jiwe la Msingi na Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kuwasili katika wilaya hiyo kesho na utazunguka katika wilaya hiyo kwa umbali wa km 304.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hii leo ofisini kwake, Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Kalisti Lazaro amesema Mwenge wa Uhuru utapokelewa Lushoto katika kijiji cha Samata kilichopo Halmashauri ya Bumbuli na utazungushwa katika halmashauri hiyo kwa umbali wa km 122 na miradi 9 yenye thamani ya Sh milioni 779 itazinduliwa.

Advertisement

Lazaro alisema kuwa miradi itakayozinduliwa na kufunguliwa na kuwekwa Jiwe la Msingi katika Halmashauri ya Bumbuli ni pamoja na miradi ya afya, elimu,maji na barabara na miradi yote imekidhi viwango na imezingatia thamani ya pesa kwa mujibu wa Sheria ya manunuzi.

Mkuu huyo alisema kuwa Juni 14 mwaka huu Mwenge utapokelewa katika Halmashauri ya Lushoto katika shule ya Msingi Kizara na utakimbizwa umbali wa km 173 katika miradi 8 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2

Alisema miradi itakayozinduliwa katika Halmashauri ya Lushoto ni pamoja na miradi ya Afya, elimu, maji na barabara yenye thamani ya kiasi hicho Cha pesa na miradi hiyo imekidhi viwango na vigezo hususani thamani ya Shilingi na kuzingatia Sheria ya Manunuzi ya Umma Kama ilivyowekwa na Serikali.

Lazaro amewataka wànanchi wote wa Wilaya ya Lushoto na viunga vyake kujitokeza kwa wingi pindi Mwenge wa Uhuru utakapopita barabarani na utakapo kwenda kuzindua miradi ya Maendeleo katika maeneo tajwa katika wilayani hiyo kwani Mwenge wa Uhuru Hauna itikadi vya vyama Bali ni Maendeleo kwa wànanchi wote wa Wilaya hiyo