MIRADI 8 ya zaidi ya Sh bilioni 1.2 itazinduliwa na kuwekwa Jiwe na Msingi katika Wilaya ya Handeni mkoani Tanga na mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Kalisti Lazaro alipokabidhiwa Mwenge wa Uhuru Kitaifa na Mkuu wa Wilaya Korogwe, Joketi Mwegelo ulipomaliza kukimbiwa katika Halmashauri ya Korogwe Vijijini.
Lazaro alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa katika Wilaya ya Handeni utakimbizwa umbali wa km 187.3 katika Kata 8 za Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na kufungua mradi mmoja,miradi miwili itatembelewa na kuonwa na miradi Murano itawekwa Jiwe la Msingi na yote itakuwa na gharama ya zaidi ya Sh bilioni 1.2
Alisema katika kuchangia gharama kutekelezwa miradi hiyo serikali kuu imetoa kiasi cha Sh milioni 728.6, Halmashauri ya Handeni imechangia Sh milioni 75.5 nguvu za Wananchi Sh milioni 271 na wahisani wamefanikiwa kuchangia zaidi ya Sh milioni 173.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa miradi itayozinduliwa, kuwekwa Jiwe la Msingi na kutembelewa ni pamoja na miradi ya maji, afya elimu na barabara yote imezingatia ubora ikiwa ni pamoja na thamani ya pesa kwa mujibu wa taratibu za manunuzi.