Mwenge wa Uhuru kuzindua miradi ya Sh bilioni 26 Kagera

MWENGE wa Uhuru mkoani Kagera unatarajia kuzindua, kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo 57 yenye thamani ya Sh bilioni 26.3.

Mkuu wa mkoa huo, Fatuma Mwasa amesema Mwenge wa Uhuru utawasili mkoani hapo Agosti 8, 2023 ukitokea Mkoa wa Geita ambapo utapokelewa Wilaya ya Muleba kata ya Nyakabango.

Alisema miradi itakayokaguliwa na kuzinduliwa ni miradi ya afya ,maji, elimu, vikundi vya vijana na wanawake, kilimo, shughuli za mapambano dhidi ya Malaria ,dawa za kulevya, lishe na kusema kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100.

Mkoa wa Kagera una halmashauri nane ambapo Mwenge huo ukihitimisha mbio zake Kagera utakabidhiwa mkoani Kigoma, ukiwa na kauli mbiu ya mbio za Mwenge¬† wa Uhuru mwaka 2023″mabadiliko ya tabia ya nchi hifadhi mazingira, tunza vyanzo vya maji, kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa taifa.

Habari Zifananazo

Back to top button