Mwenge wa uhuru wakagua miradi ya Sh bilioni 1 Nanyumbu

MWENGE wa Uhuru ukiwa wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara umekagua miradi 13 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh.

Bilioni 1.

Akizundua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa vyumba viwili vya madara shule ya sekondari ya Mikangaula wilanyani humo, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim amegundua kuwepo kwa baadhi ya dosari kwenye mradi huo.

Baadhi ya dosari hizo ambazo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amezigundua katika mradi huo ikiwa ni pamoja na vioo, vitasa, malumalu (Tailis) kutokana na kukosa ubora unaostahili huku akitoa wiki tatu kwa wataalam wa halmashauri hiyo kuhakikisha dosari hizo zinafanyiwa maboresho kupitia gharama zao na siyo za Serikali mradi ambao umegharimu Sh miliomi 40.

“Natoa wiki 3 kuhakikisha hizi dosari zinarekebishwa kwa kutumia gharama zenu ili kuleta ubora wa madarasa haya na wanafunzi waweze kusoma katika mazingi mazuri lakini pia kuufanya mradi huu uwe imara kwa mrefu “,

Aidha, licha ya kuwepo kwa dosari hizo kwenye mradi huo lakini pia Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru ameridhia kufungua, kuweka jiwe la msingi kwenye mradi huo kwani umekidhi vigezo na ubora unaostahili.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Yohana Mlawa amesema mradi huo ulianza kutekelezwa Novemba 2022 na kukamilika Disemba 2022 ambapo umekamilika kwa asilimia 100 mpaka sasa.

Amesema mradi huo utasaidia kupunguza upunguza wa madarasa na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kujifundishia.

Baadhi ya wanafunzi shuleni hapo akiwemo Fahamu Hassan kutoka kidato cha nne ameishukuru Serikali kuwajengea madarasa hayo kwani kutawaongezea bidii katika masomo yao na kuleta ufaulu mzuri.

Bahati Mohamedi kutoka kidato cha kwanza shuleni hapo “ujenzi wa madarasa haya itakuwa tija kwa sisi wanafunzi kujifunza vizuri na umakini wa hali ya juu kwahiyo tunaipongeza sana Serikali yatu kwa kutuboreshea kwenye elimu ili tuweze kusoma katika mazingira mazuri na Bora”,

Habari Zifananazo

Back to top button