MWENGE wa Uhuru umeingia mkoani Kagera, ambapo kilele chake itakuwa Oktoba 14 mwaka huu na mgeni rasmi atakuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yamefanyika katika Kijiji cha Nyamigere, Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera, ambapo <kuu wa Mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye, alimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila Mwenge huo wa huuru.
Kwa mujibu wa Chalamila mwenge huo ukiwa mkoani Kagera utazindua, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo 37 yenye thamani ya Sh Bilioni 13.
Baada makabidhiano hayo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, alikabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Kemilembe Rwota.