Mwenge wapitia miradi mitano Tandahimba

MIRADI mitano yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 4, imewekewa Jiwe la Msingi na Mwenge wa Uhuru wilayani Tandahimba.

Miongoni mwa miradi hiyo ni kiwanda cha kubangua korosho cha Organic Growth Limited wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya mwenge huo kuwasili katika wilaya hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Mussa Gama amesema miradi hiyo iko vizuri, ambapo mitatu itawekewa jiwe la Msingi na miwili itazinduliwa.

Meneja wa kiwanda hicho cha kubangua korosho, Hassan Bakari  amesema kiwanda kimekamilika kwa asilimia 95 na kimegharimu zaidi ya Sh Bilioni 3, ambapo kitakuwa na uwezo wa kubangua tani 8 mpaka 10 za korosho ghafi kwa siku na tani 3,000 korosho karanga kwa mwaka na kitatoa ajira 150 za muda na 50 za kudumu.

Amesema kiwanda hicho kinatarajia kuanza kazi Mei mwaka huu na kinatarajia kuongeza ajira kwa Watanzania.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Abdallah Shaib Kaim amepongeza kazi hiyo mzuri ya uwekezaji iliyofanyika katika ujenzi huo.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x