Mwenye kilo 145 afanyiwa upasuaji kupunguza uzito

DAR ES SALAAM; MTUMISHI wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, amefanyiwa upasuaji mdogo wa kukatwa utumbo wa chakula kupunguza uzito katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili- Mloganzila.

Mtumishi huyo wa jinsia ya kike (32) alikuwa na kilo 145 na amekatwa utumbo, ili aweze kufikia kilo chini ya 80.
Gharama za upasuaji huo mdogo ni Sh milioni 15, ambazo zimelipwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza leo Februari 29, 2024 Daktari Bingwa wa Upasuaji na Mkuu wa Idara ya Upasuaji, Eric Muhumba amesema upasuaji huo umetumia saa moja na kwamba mgonjwa huyo amelazimika kufanya upasuaji huo kutokana na kuwa na changamoto ya kupumua.

“Upasuaji tuliofanya ni wa kukata sehemu ya kipande cha utumbo, hiyo inamfanya mtu atumie chakula kidogo ukilinganisha na awali hatua itakayomuwezesha apungue uzito,”amesema na kuongeza:

“Upasuaji huu ni wa moja kwa moja ‘permanent’, mtu akifanyiwa hawezi tena kurudi kuwa mnene, sio kama puto ukiwekewa ukatolewa, usipozingatia mtindo bora wa maisha unarudia tena unene,”amesema.

Habari Zifananazo

Back to top button