Mwenye ulemavu wa kusikia atesa shindano la hisabati

YUSTER  Sanga ambaye ana ulemavu wa kusikia ameibuka kidedea kwa kuongoza somo la hisabati katika shindano la umahiri kwa vijana wanaoshughulikia ufundishaji lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) kupitia shule kuu ya elimu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa utoaji tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri, Kaimu Makamu Mkuu wa chuo hico  anayeshughulikia utafiti, Nelson Boniface amesema faida ya shindano hilo ni kuwapima wanafunzi.

“Ni shindano la kwanza katika chuo chetu na tumeshirikiana na chuo cha Zhehang  Normal kutoka nchini China, ambacho wao wanayafanya shindano hili kwa mwaka wa 8 sasa.

“Shindano haya yalikuwa yakihusisha masomo ya hisabati, Kiswahili, Biologia, Geographia na Physical ambapo binti mwenye uhitaji maalumu amekuwa kidedea kupitia somo la hisabati.

“Hii inaonesha kwa kiasi gani walemavu wana uwezo wa kufanya makubwa ukizingatia ukubwa wa somo aliloongoza tutoe fursa kwa wengine wenye uhitaji na wamekosa nafasi UDSM milango ipo wazi chukueni fursa,”amesema Boniface.

Kwa upande wake mshauri wa wanafunzi Dk Eugenia Kafanabo, amesema mashindano haya yaliandaliwa mahususi kupata taarifa kutoka kwa watu mbalimbali na kukusanya maoni kuhusu wanafunzi, ili kujua changamoto za wanafunzi.

“Majaji wa shindano hilo walikuwa walimu wa sekondari binti aliyeshinda kwenye mahesabu na kuwa wa kwanza ni mfano wa kuigwa kwa wanafunzi wengine na changamoto zitafanyiwa kazi, “amesema.

Naye mwanafunzi mwenye ulemavu wa kusikia Yester Sanga amesema kuwa anashukuru kwa zawadi na nafasi aliyopewa amefurahia kuona walemavu wanapewa fursa.

“Niwaombe nafasi tumeshapata wajitokeze kwa wingi kwenye mashindano nasi tunaweza  walemavu tuingie tupambane tutashinda,”amesema

Habari Zifananazo

Back to top button