Mwenyekiti CCM alia kuchafuliwa

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joas Muganyizi Zachwa amelia kuchafuliwa kwa kuhusishwa kutukana madiwani.

Akizungumza na HabariLEO Zachwa amesema kuwa wapo baadhi ya watu wanamtengenezea ajali ili ang’,oke katika nafasi hiyo.

“Kuna clip ya audio nimeona kuwa niliwatukana madiwani na katibu wangu wa zamani wa Chama. Clip hile niyakutengenezwa.” Amesema Zachwa

Advertisement

Amesema tayari ameanza kuchukua hatua za kisheria na kutaarifu vyombo vinavyohusika kushughulikia.

“Najua hii inafanyika kutokana na mimi kusimamia maelekezo ya Ilani ya CCM na misingi ya chama chetu ya kushughulikia kero za wananchi hasa wafanya biashara. Nataka niwahidi wanaCCM wa Wilaya ya bukoba mjini, CCM na serikali yake itabaki kuwa salama.” Amesema

Aidha, amesema hatosita kuwasemea wananchi kwani ndio maelekezo ya Ilani na viongozi wakuu wa Chama hicho tawala.