Mwenyekiti CCM auawa Katavi

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kamsisi Halmashauri ya Mlele Mkoa wa Katavi, Leonard Frank, mwenye umri wa miaka miaka 51 ameuawa kwa kukatwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu kinachodhaniwa kuwa ni panga usiku wa Februari 21 2023.

Mauaji hayo yamedaiwa kutekelezwa na watu wasiofahamika usiku, ambao walifika nyumbani kwa marehemu na kumtaka kutoa fedha kabla ya kufanya mauaji hayo.

Kwa upande wake mtoto wa marehemu, Geofrey Frank amesema hawakuwahi kusikia baba yao kama ana migogoro ama ugomvi na mtu yeyote, huku wakiiomba Serikali kutolifumbia macho suala hilo.

Akizungumza keneo la msiba, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga amewaagiza maofisa usalama wilayani hapo kwa kushirikiana na viongozi wa jadi pamoja na sungusungu kukomesha matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara wilayani hapo.

Naye Diwani wa Kata ya Kamsisi, Leonard Kiyungi amesema, ameupokea kwa masitiko makubwa msiba huo kwani ni muda mfupi tu baada ya Katibu wa CCM wa Kata hiyo kufariki kutokana na ajali ya gari.

Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, imetoa gari kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea nyumbani kwao mkoani Geita kwa mazishi.

Habari Zifananazo

Back to top button