Mwenyekiti UVCCM Arusha Mjini afanya ziara Baraa

MWENYEKITI Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Arusha Mjini, Hassan Mndeme ameongoza wajumbe wa kamati ya utekelezaji kufanya ziara ya uimarishaji wa Jumuiya katika kata ya Baraa iliyopo Wilaya ya Arusha Mjini mkoani Arusha.

Ziara ya Mwenyekiti imeanza kwa kufanya kikao cha ndani na viongozi na wanachama wa Jumuiya kata ya Baraa na kukutana na makundi mengine ambayo yanamfungamano na jumuiya ya vijana.

Ziara hiyo pia imehusisha kutembelea kituo cha kutolea mafunzo kwa mabinti waliopewa ujauzito katika umri mdogo ili waweze kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa kujitegemea kupitia ujuzi wanaopewa kituoni hapo.

Akiwa kituoni hapo Mndembe ameahidi kuendelea kushirikiana na uongozi wa kituo kwa kuwapeleka wadau mbalimbali ili kuweza kusaidia katika kukidhi baadhi ya mahitaji ya msingi kwa kituo hicho pia ametembelea makundi mbalimbali ya vijana kama bodaboda na wajasiriamali na kuzindua mashina ya wakereketwa katika maeneo yao.

Habari Zifananazo

Back to top button