MWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),William Rhys Mahalu amefaiki dunia.
Taarifa iliyolewa mapema leo na taasisi hiyo imesema: “Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dk Peter Kisenge anasikitika kutangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi hiyo Prof. William Rhys Mahalu kilichotokea jana usiku wa tarehe 20/08/2023 katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alikokuwa anapatiwa matibabu,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Comments are closed.